Kuona ni kuamini ; Seeing is believing (Documentary Script) 15th April 2024 Published and All rights reserved here.

IMG_6404.JPGKuona ni kuamini ; Seeing is believing 

(Documentary Script)


All rights reserved 2019


Episode1

Written by J.M.Samwel, Optometrist 

T/A Optsam

2019


Mathayo 6:22

“Jicho ni taa ya mwili. Kama basi jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga.”


Oxford’s language Dictionary 

See

To perceive with the eyes; discern visually.

Believe 

To accept that (something) is true, even if you don’t have proof 


Optsam : Seeing is believing 


Kuona ni kutambua na kukubali kuwa ni kweli sasa..


Idadi ya watu vipofu duniani inaongezeka kwa kasi zaidi kuliko idadi ya watu duniani inavyoongezeka.


Angalau watu bilioni 2.2 wana matatizo ya uoni, na kati yao, angalau watu bilioni 1 wana matatizo ya kuona ambayo yanaweza kuzuilika au bado 


Samwel John, 26,Tanzanian Optometrist T/A Optsam eye care and optical workshop store ©️2019 (Check Optsam®️ Bio.)


Watu wengi wanachagua bila hiari/ bila kufahamu kutoshughulika na afya za macho yao kutokana  na kuhisi kuona bado wanaweza kuendelea na shughuli zao wanazofanya kila siku bila vikwazo.


Jicho ni kiungo chenye muundo wa ajabu na mgumu kujifunza katika mwili wa binadamu. 


Macho mawili hutoa karibu nusu ya hisia zote za mwili mzima kuelekea kwenye ubongo kwa ajili ya  kuona.


Hatuoni kwa macho tunaona kwa ubongo

Utambuzi hufanyika katika ubongo hivyo, Jicho ni zana hutumika kwa ajili ya kuona kupitia kichochezi ambacho ni Mwanga


Mwanga ukifika kwenye “pazia la kuona” (Retina) hubadilishwa na kuwa mfumo wa taarifa za fahamu na “seli maalum” kupitia mshipa wa fahamu (Neva ya Optika) na kupelekwa kwenye ubongo kwa ajili ya utambuzi.


Jicho ni kiungo cha nje na hivyo kinakabiliwa sana na mazingira. Kwa hiyo, usafi duni pamoja na lishe,hali ya hewa, wadudu wanaosambaza magonjwa,kuongezeka kwa idadi ya watu,kuzeeka pamoja na mitindo ya maisha, na vingine huchangia kuathiri kwa kiasi kikubwa idadi na aina ya magonjwa ya macho katika jamii.


Nimekuwa nikifanya kazi ya optometria tangu mwaka 2017 kama huduma katika ngazi ya awari/msingi ya utunzaji wa macho ambayo ni uchunguzi wa uoni, utoaji wa miwani tiba, kutambua na kusimamia magonjwa ya macho au kutoa rufaa kwa wataalamu wengine.


“Kuona ni kuamini” ilibuniwa ili kuleta mwanga na sauti itakayowawezesha na kushirikisha watu katika jamii zote zaidi kuhusu elimu ya afya ya macho kama zana kwa ajili ya kuona kupitia programu endelevu kama ilivyopendekezwa na @who kwenye ripoti yake ya World Vision ya mwaka 2020©️. 

Programu hizi zitawashirikisha watu binafsi na familia katika jamii zote kwa kuamini katika kuzuia, kufanya maamuzi na kuhusika kujisimamia kuhusu uwezo wa macho yao kuona.


Watu wakipata elimu kuhusu macho yao , itawaaminisha wao ni wa kwanza kugundua na kuchukulia hatua kila wanapohisi dalili kabla ya ugonjwa kutokea 


Ikiwa macho yetu hayapokei mwanga kwa muda mrefu, yanaweza kuzorota na kusababisha hatari kubwa ya upofu au uoni hafifu. Hali hii inaweza kuchukuliwa kama ulemavu, 


Mtu anaweza kuwa mlemavu wa kuona bila kufahamu na bado akawa na uwezo wa kutembea bila kikwazo/msaada ( Uoni Hafifu ) i.e Albino. 



Episode 2


Overview

Kupitia picha za kuvutia na mahojiano ya wataalamu, Makala hii itatoa uchunguzi wenye maarifa na fupi juu ya jinsi ubongo wetu unavyochakata taarifa za kuona, macho kama zana ya kuona, na hatari na changamoto zinazohusiana na uoni kwa ujumla Duniani.


Katika Makala hii, tutaelezea dhana ya jinsi tunavyoona kwa ubongo wetu badala ya macho yetu. Macho yetu hutumika kama zana ya kuona, lakini yanahitaji vichocheo kutoka nje, ambacho haswa Mwanga, ili kufanya kazi kwa ufanisi. Kama vile gari linahitaji mafuta ili kuendeshwa na mtu, macho yetu yanahitaji mwanga kama chanzo cha nishati ili kutambua vitu katika shughuli zetu za kila siku.


Ulemavu ni hali yoyote ya mwili au akili (upungufu) ambayo inafanya iwe vigumu kwa mtu mwenye hali hiyo kushindwa kufanya shughuli fulani (ukomo wa shughuli) na kuwasiliana na ulimwengu unaonzunguka (vikwazo vya ushirikiano).


Mtu anaweza kuwa mlemavu wa kuona bila kufahamu na bado akawa na uwezo wa kutembea bila kikwazo/msaada ( Uoni Hafifu ) i.e Albino. 


Pua yako huwa unaingalia lakini ubongo wako hauoni kupitia mchakato unaoitwa kitaalamu “Unconscious selectively” uchaguzi bila hiari/ bila kufahamu .


Huoni pua yako kwa sababu ubongo wako hauishughulikii. Ingawa pua yako iko muda wote katika uwanja wako wa kuona, ubongo wako unaiacha kwa sababu sio taarifa unayohitaji kufanyia  katika shughuli za kila siku.


Hatuoni kwa sababu hatushughuliki na Taa inayomulika mwilini”(jicho) na badala yake ubongo unashindwa kupata vizuri taarifa muhimu huihitaji kufanyia kazi katika shughuli zetu za kila siku kwa ajili ya kuona ambayo ni “Mwanga” 


Lesson 


Upofu

Upofu unaweza kutokea ghafla au taratibu huku ikitegemeana na kisababishi.


Kulingana na WHO,Upofu ni uwezo wa kuona chini ya 3/60 kwa jicho bora pamoja na miwani inayofaa zaidi, au upotezaji wa upeo wa kuona chini ya 10 katika uwanja wa kuona. (Upotevu huu wa upeo wa macho unazuia mtu kutembea au kujiongoza kwa uhuru).


Uoni Hafifu

Pia kuna kundi jingine la watu wenye "uoni hafifu" ni uwezo wa kuona chini ya au 6/18 lakini bora kuliko 3/60 kwa jicho bora pamoja na miwani inayofaa zaidi. (Mtu huyu anakuwa na  ulemavu wa kuona lakini anaweza kuzunguka kwa uhuru kabisa).


Mzigo huu haukubebwa sawasawa. Unawalemea zaidi jamii zenye kipato cha chini na cha kati, pamoja na watu wazee, na jamii za vijijini.


Jamii maskini au jamii zinazoendelea, huwa na huduma duni za matibabu na hivyo magonjwa mara nyingi huonekana katika hali mbaya au husahaulika kushughulikiwa.



Watu wanaohitaji huduma ya macho lazima waweze kupata huduma bora, zinazopatikana na kufikika katika maeneo yote ya jamii pasi na kupitia ugumu kifedha.


IMG_5885.JPG


Malengo yake yanazingatia magonjwa yanayosababisha upofu unaozuilika na kutibika.

i. Kutekeleza IPEC kwa kutoa huduma bora za afya ya macho ambazo zinapatikana na kufikika katika maeneo yote ya jamii.

ii. Kuwezesha jamii za ndani kupokea huduma bora za afya ya macho bila kuteseka kifedha.

iii. Kuwawezesha na kuwashirikisha watu katika jamii kwa kutekeleza programu endelevu za afya ya macho.

iv. Kutoa huduma za afya ya macho zilizoandaliwa vizuri kupitia usimamizi wa kesi, huduma kitimu na mfumo mzuri wa rufaa.


How Optsam operates;

Visiting care

Visiting Doctor/Optometrist that provides a mobile eye care by screening and assessing people in all community settings and give them medical/optical care, those needing more intensive management are then referred to other specialists (Tertiary health care).


Jinsi Optsam inavyofanya kazi;

Huduma ya kutembelea

Kuna Daktari/Mganga anayetoa huduma ya afya ya macho kwa kutembelea.

Huchunguza na kutathmini watu katika jamii na kuwapa huduma za matibabu au ushauri, wale wanaohitaji huduma za uangalizi zaidi hupelekwa kwa wataalamu wengine (huduma ya afya ya ngazi ya juu).


Eye Health Literate care and Training 

“Seeing is believing “  was invented to bring the light and sound that will empower and engage people in all communities about eye health education through sustainable programs as @who recommended on its previous World Vision report 2020©️

These programs engage individuals and families “believing” in prevention, decision making and self-management concern their eyes ability to “see(ing)”.


Skilled based Training within Optometry premises i.e Media Interviews, Visual Acuity Concept. , Presentations, Podcasts , Documentaries etc.



IMG_8146.jpeg


IMG_6404.JPG


Optsam store

This is an Optical workshop store deals with health and beauty , It provides the selling products and services including therapeutic lenses, cosmetic lenses, brandy frames, spectacles, contact lens fitting, optical accessories etc.


As we reflect on the powerful words of Surah An-Nur Ayat 35 from the Quran, we are reminded that.


“Allah ni Nuru ya mbingu na dunia. Nuru yake ni kama tundu ambayo kuna taa, taa iko katika kioo, kioo ni kama nyota inayong'aa, iliyoung'aa kutokana na mafuta ya mzeituni mwenye baraka, wala haiko upande wa mashariki wala magharibi, ambayo mafuta yake yanaweza kuwaka hata bila kuguswa na moto. Nuru juu ya nuru! Allah anamwongoza yeyote anayemtaka kwenye nuru yake. Na Allah anaweka mfano kwa ajili ya binadamu. Kwani Allah anajua kila kitu kwa ukamilifu.”


With this profound message, we find hope in the increasing awareness of the challenges of treatable and preventable blindness in our world. Governments have formed committees to address the issue on a local level, while funds from organizations like the World Bank support cataract surgeries in countries like India. Moreover, there is a growing recognition of the importance of training and supporting paramedical staff, such as ophthalmic medical assistants, to initiate eye programs.


However, despite these efforts, the number of avoidably blind individuals continues to rise at a faster rate than the world population. It is crucial that we acknowledge this alarming trend and take decisive action to combat it.


Utabiri unaonyesha kuwa mahitaji ya huduma ya macho duniani yataongezeka katika miaka ijayo kutokana na ukuaji wa idadi ya watu, kuzeeka, na mabadiliko katika mtindo wa maisha.


In the words of J.M. Samwel, a dedicated optometrist, "Seeing is believing." Let us strive together to ensure that everyone has the opportunity to see the world and experience its wonders. Only then can we truly make a difference and bring light to the lives of those who need it most.


Comments

Popular posts from this blog

Swift Charitable Mobile Eye Clinic at Kilamba primary school, Mbagala Charambe