Kama mtaalamu wa afya ya macho, ninaamini kuwa kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kunahitaji uwekezaji imara katika afya ya macho kama sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa. Maono yangu ni kuona Tanzania ambayo kila mwananchi anapata huduma bora, nafuu na zinazopatikana kwa wakati, bila kujali hali yake ya kiuchumi au mahali anapoishi. Kuelekea mwaka 2050, tunapaswa kuimarisha maeneo matano muhimu: πΉ Bima ya Afya kwa Wote — kuhakikisha vipimo, matibabu na huduma za kurekebisha uoni zinawafikia wananchi wengi zaidi. πΉ Kuzuia Upofu Unaoweza Kuepukika — kuimarisha uchunguzi wa mapema, elimu ya afya ya macho na upatikanaji wa miwani. πΉ Teknolojia na Akili Mnemba (AI) — kutumia ubunifu wa kidijitali kuboresha uchunguzi na kuunganisha huduma za macho, hasa katika maeneo ya vijijini. πΉ Kuongeza Wataalamu na Uwezo wa Huduma — kujenga nguvu kazi yenye ujuzi wa kutosha katika ngazi zote za mfumo wa afya. πΉ Ushirikiano wa Kimkakati — kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, wataalamu, sek...